Kaimu Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala akizungumza na wazazi, wanafunzi na viongozi na wadau wa elimu katika mkutano wa majumuisho mara baada ya washiriki wa juma la elimu kutembelea shule za msingi Mgusu na Mshikamano pamoja na Shule ya Sekondari Mgusu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita.

Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji wa Geita, Bi. Linda Marandu akizungumza
na wazazi, wanafunzi na viongozi na wadau wa elimu katika mkutano wa majumuisho mara baada ya washiriki wa juma la elimu kutembelea shule za msingi Mgusu na Mshikamano pamoja na Shule ya Sekondari Mgusu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita.


Baadhi ya wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wadau wa elimu wanaoshiriki Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita wakiwa katika majadiliano na wanafunzi.

Afisa Elimu Watu Wazima Mkoa wa Geita, Bi. Salome Cherehani akizungumza na wazazi, wanafunzi na viongozi na wadau wa elimu katika mkutano wa majumuisho mara baada ya washiriki wa juma la elimu kutembelea shule za msingi Mgusu na Mshikamano pamoja na Shule ya Sekondari Mgusu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita.

Baadhi ya wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wadau wa elimu wanaoshiriki Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita wakiwa katika majadiliano na wanafunzi.


Kaimu Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala akisisitiza jambo alipokuwa kwenye mkutano na wazazi, wanafunzi na viongozi na wadau wa elimu katika mkutano wa majumuisho mara baada ya washiriki wa juma la elimu kutembelea shule za msingi Mgusu na Mshikamano pamoja na Shule ya Sekondari Mgusu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Juma la Elimu Kitaifa, ambaye pia ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Uwezo Tanzania, Bw. Greyson Mgoi (kulia) akizungumza kuwatambulisha wadau wa elimu walipotembelea baadhi ya shule ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yaliofanyika Mkoani Geita.

KAIMU Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala amewataka wazazi na walezi wa wanafunzi katika shule za msingi Mgusu na Mshikamano pamoja na Shule ya Sekondari Mgusu kuhakikisha wanafunzi katika shule hizo wanapata chakula wawapo shuleni.

Kauli hiyo, imetolewa leo mkoani Geita katika ziara ya wadau wa elimu wanaoshitiki Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita, walipokuwa wakizitembelea shule hizo na kuzungumza na wazazi, wanafunzi, walimu pamoja na viongozi na wadau wa elimu. 

Alisema haki ya mtoto kupata chakula ni ya msingi hivyo ni jukumu la wazazi na walezi kuhakikisha wanakula ili waweze kusoma vizuri na hata kufaulu katika masomo yao, kwani mtoto akiwa na njaa hawezi kusoma na kuelewa kwa urahisi anachofundishwa na walimu.

"Naomba sana wazazi na walezi tuhakikishe kwamba watoto wetu wanakula wakiwa shuleni kwani watoto hawa muda mwingi wanautumia wakiwa shuleni tukiwaacha watoto hawa wakakaa na njaa wakiwa shuleni tunatengeneza matatizo ya kiafya kwao kama vidonda vya tumbo naomba tuchangie ili tuwanusuru," alisema Kaimu Mratibu wa TEN/MET, Bi. Makala akizungumza.

Aliongeza kuwa kiasi kinachotakiwa kuchangiwa kwa kila mzazi ni kilo moja ya mahindi na shilingi mia tano (500) tu kwa mwezi kiwango ambacho kinaweza kuchangiwa kwa kila mzazi kama amedhamiria kufanya hivyo. Kuna watoto 687 wanashinda na njaa kila siku wawapo shuleni huku wenzao 813 wanapata huduma ya uji shuleni kila siku. 

"...Ni vizuri mtoto asome akiwa ameshiba hapa anaweza kumsikiliza mwalimu vizuri, lakini tumboni akiwa hana kitu hawezi kumsikiliza mwalimu na kuelewa kirahisi...kwa hili nawasihi wazazi tusaidiane, Serikali inajitahidi kufanya kwa sehemu yake lakini wazazi na wadau wengine tuna kila sababu ya kuunga mkono juhudi hizo za Serikali"

Aidha aliongeza kuwa ushirikiano kati ya wazazi, walimu na viongozi wa elimu ndio njia pekee inayoweza kuchochea maendeleo ya elimu katika eneo hilo. 

Kwa upande wake, Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji wa Geita, Bi. Linda Marandu alisema licha ya uwepo wa changamoto hiyo ya baadhi ya wazazi kutoitikia uchangiaji wa chakula eneo hilo, lakini bado Kata ya Mgusu inaongoza kufanya vizuri katika uchangiaji chakula ukilinganisha na kata zingine eneo hilo. 

Baadhi ya walimu wakizungumza na wadau wa elimu walipofanya ziara katika shule hizo.

Baadhi ya wazazi na wanafunzi wakiwa katika vikao na wadau wa elimu.

Baadhi ya wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wadau wa elimu wanaoshiriki Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita wakiwa katika majadiliano na walimu.

Baadhi ya wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wadau wa elimu wanaoshiriki Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita wakiwa katika majadiliano na wanafunzi wa shule za msingi.

Kwa muda mrefu kinamama waliokuwa wanajifungua watoto kabla ya wakati (njiti) wamekuwa wakipatwa na hofu na mashaka kuhusu mustakabali wa maisha ya watoto wao kwakuwa inaelezwa wengi wa watoto hao walikuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa huduma bora za uangalizi kwa mama na mtoto.

Hata hivyo jambo hilo kwa sasa linaonekana kuwa historia kutokana na maboresho ya mifumo ya kitaalamu na uwepo wa Madaktari Bingwa wabobezi kwenye Hospitali mbalimbali za umma hapa nchini ambapo uangalizi dhidi ya watoto hao umekuwa ukifanywa kitaalamu zaidi.

Hilda Msigwa mkazi wa mkoa wa Songwe na Rose Masebo mkazi wa mtaa wa Mabatini Mbeya ni miongoni mwa kinamama mashuhuda, ambapo wawili hao kwa sasa wamelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wakipatiwa uangalizi maalumu wa huduma ya Kangaroo baada ya kujifungua watoto wao kabla ya wakati (njiti) .

Katika maelezo yao wamesema kuwa watoto wao wamezaliwa wakiwa na gramu tano (5) ndani ya kipindi cha miezi miwili (2) pekee watoto hao wamefikisha kg 1.5 jambo ambalo limewapa faraja kubwa.

Wametumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyofanikisha mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya nchini ambayo yameokoa maisha ya watoto wengi waliozaliwa kabla ya wakati (njiti)




 

Na Mwandishi Wetu,Dodoma.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amepokea msaada wa 13.7m/- kutoka kwa wanachama wa kundi sogozi(WhatsApp) liitwalo Viongozi Tanzania.

Akipokea msaada huo katika hafla hiyo iliyofanyika jana ofisini kwake Mei 6,2024,mjini Dodoma ,Dkt Yonazi amewashukuru wanachama wa kundi hilo kwa kujitoa kwao kwenda kwa waathirika hao wa maporomoko ya udongo, tope, mawe na magogo kutoka mlima Hanang mkoani Manyara yaliyotokea mwishoni mwa mwaka 2023.
Dkt.Yonazi amesema msaada huo,pamoja na misaada ya wasamalia wengine inaunga mkono jitihada za serikali zinazoendelelea katika kurejesha hali ya kawaida kwa waathirika hao ikiwemo kujengea nyumba 108, ili wanaendelee kujitafutia riziki na kujiletea maendeleo yao.

Aidha, Dkt. Yonazi ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kuwa na desturi ya kuwakimbilia wahitaji pale ambapo wanapata athari za majanga mbalimbali.

"Tunawashukuru wenzetu wa kundi la Viongozi Tanzania kwa uzalendo waliouonesha kwa ajili ya mchango huu mkubwa walioutoa, niwaombe Watanzania wenzangu tuzidi kushikana mkono hasa nyakati hizi ambapo sehemu nyingi nchini yametokea majanga mbalimbali,hivyo ni  jambo jema kuendelea kushirikiana kuwasaidia ndugu zetu, "alisema Dkt. Yonazi

Wajumbe wawili wa kundi hilo ambao ni Ndg.Benjamin Thompson, ambaye ndiye Mratibu Mkuu wa kundi hilo, pamoja na Mhandisi Archard Kato,ambaye ni mmoja wa Wanachama wa kundi hilo, waliwawakilisha wanachama wengine zaidi ya 600 walioko kwenye kundi hilo, ambao ni viongozi mbalimbali wa serikali,viongozi wa taasisi za umma,viongozi wa sekta binafsi,wahadhiri na viongozi wa vyuo vikuu,viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wadiaspora n.k

Bw.Thompson alisema michango hiyo ilikusanywa kutoka kwa wanachama 145 tu kati ya wote walioko kwenye wa kundi hilo, ambao ndio waliweza kuchangia kwa wakati huo.
"Mkusanyaji wetu alikuwa ni Zamaradi Kawawa,ambaye alifanya kazi nzuri sana na kwa uaminifu mkubwa.Baada ya kumaliza kazi hiyo,tulikubaliana kwamba aweke pesa hizo kwenye akaunti ya maafa iliyopo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu,na aliweka pesa hizo Desema 27,2023.Sasa hili lililofanyika hapa leo lilikuwa ni kukabidhi tu karatasi ya malipo yaani pay in slip",alisema Bw Thompson.

Naye Mhandisi Kato,  ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya kutengeneza mvinyo ya Alko Vintages iliyopo Dodoma, alisema wanachama wa kundi hilo wameguswa na janga hilo la Hanang na hivyo kuona umuhimu wa kutoa michango hiyo katika kuunga mkono juhudi za serikali za kukabiliana na majanga kama hayo.
"Tunakuahidi kwamba tutaendelea kuisaidia serikali kwa kidogo tulicho nacho katika kukabiliana na athari za majanga kama haya,na tungependa kuona hili jambo linaenea kwa watanzania wengi,yaani hata kabla ofisi yako haijafika au serikali haijafika, angalau watanzania wenyewe wawe wanafanya jambo la mwanzo kwa uzalendo wao katika kukabiliana na mambo hayo hasa ya dharula ambayo hakuna mtu ambaye amepanga yatokee hasa hasa mafuriko,"alisema Mhandisi Kato.

Janga la Hanang lilitokea Desemba 3, mwaka jana mkoani Manyara na kusababisha vifo ya watu zaidi ya 80, huku mamia wengine wakiachwa bila makazi, uharibifu mkubwa wa miundombinu.




 

 

 

Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Dk. Zelia Njeza (kulia) pamoja na Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wanaosomea masomo ya Ukaguzi wa Ndani UDSM, IAA, Bi. Daines Mbao wakipongezana mara baada ya kusaini hati za makubaliano ya kuchochea vipaji vya wanafunzi wanaosomea masomo ya Ukaguzi wa Ndani UDSM na vyuo vingine.

Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Dk. Zelia Njeza (katikati) pamoja na Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wanaosomea masomo ya Ukaguzi wa Ndani UDSM, IAA, Bi. Daines Mbao (wa kwanza kushoto) wakisaini hati za makubaliano ya kuchochea vipaji vya wanafunzi wanaosomea masomo ya Ukaguzi wa Ndani UDSM na vyuo vingine. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa IIA, Bw. Jonathan Ngoma akishitiki tukio hilo.

Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Dk. Zelia Njeza (kulia) pamoja na Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wanaosomea masomo ya Ukaguzi wa Ndani UDSM, IAA, Bi. Daines Mbao wakipongezana mara baada ya kusaini hati za makubaliano ya kuchochea vipaji vya wanafunzi wanaosomea masomo ya Ukaguzi wa Ndani UDSM na vyuo vingine.

Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Dk. Zelia Njeza, akizungumza wakati wa hafla ya kutiliana saini ya baina ya Jumuiya ya Wanafunzi wanaosomea masomo ya Ukaguzi wa Ndani UDSM. Kushoto ni Rais wakilishi wa Jumuiya ya wanafunzi hao Bi. Daines Mbao

TAASISI ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA) imesaini makubaliano na Jumuiya ya Wanafunzi wanaochukua masomo ya Ukaguzi wa Ndani Chuo Kikuu cha UDSM lengo likiwa ni kuchochea vipaji na hamasa kwa wanafunzi kujiunga na fani hiyo mapema zaidi wawapo vyuoni. 

Hafla ya kutiliana saini ya pande hizo mbili imefanyika juzi jijini Dar es Salaam, ambapo Jumuiya ya Wanafunzi wanaosomea masomo ya Ukaguzi wa Ndani UDSM IAA iliwakilishwa na Rais wa Jumuiya hiyo, Bi. Daines Mbao huku Taasisi ya IIA ikiwakilishwa na Rais wake, Dk. Zelia Njeza.

Akizungumza katika hafla hiyo, iliyofanyika sambamba na utambulisho wa Maadhimisho ya Mwezi wa Wakaguzi wa Ndani, yaani Mwezi Mei wa kila mwaka, Rais wa IIA, Dk. Njeza alisema makubaliano hayo yatasaidia kuhamasisha vijana wengi kujitokeza na kujiunga na masomo ya ukaguzi wa ndani tangu wawapo vyuoni.

Alibainisha kuwa IIA pamoja na IAA zitatumia Mwezi huu wa wakaguzu wa ndani kukuza na kuchochea vipaji vipya vya wakaguzi wa ndani kuanzia ngazi za elimu ya vyuo vikuu, kuwajengea uwezo zaidi na hamasa kusomea masomo hayo ili kupata wataalamu wengi zaidi wa fani hiyo hapo baadaye. 

Alisema viongozi na wataalamu watazunguka sehemu mbalimbali kutoa elimu kupitia vyombo vya habari na baadhi ya vyuo vikuu lengo likiwa ni kuchochea vijana shuleni kujiunga na fani hiyo ambayo inaumuhimu mkubwa kwenye maeneleo ya taasisi na taifa kwa ujumla.

"Tutawaelezea hasa wanafunzi vyuoni umuhimu wa fani ya ukaguzi wa ndani na namna gani wanaweza kufikia kuwa wakaguzi endapo watavutiwa na fani hiyo. Lakini pia sisi kama wakaguzi wa ndani tunamiongozo mbalimbali ambayo hutumika tunapokuwa tukitekeleza majukumu yetu. 

"Mwezi huu wa tano ni mwezi wa wakaguzi wa ndani, nasi kama wakaguzi wa ndani wa Tanzania tunajumuika na wakaguzi wenzetu ulimwenguni kusherehekea mwezi huu, Tunasherekea kwa namna mbalimbali ikiwemo kuweza kutambua mchango wa wakaguzi wa ndani kwa jamii, kwa taasisi na kwa taifa kwa ujumla."

Aidha pamoja na mambo mengine watatumia muda huo kutafakari kazi zetu huku tukiangalia mabadiliko mbalimbali yanayojitokeza katika mazingira ambayo tunafanyia kazi, licha ya kutambua kuwa kuna changamoto nyingi katika mazingira tunayofanyia kazi zetu huu ni muda muafaka wa kutoa elimu kwa wadau wetu.

Alibainisha kuwa mwongozo mpya wa shughuli za ukaguzi wa ndani uliopitishwa kutumika duniani kote utaanza kutumika Januari mwakani ili kupata viwango sawa vya ukaguzi maeneo yote, hivyo watatumia mwezi huu Mei kutoa elimu kwa wadau wao na wana tasnia juu ya kanuni mpya na namna ya kuzitumia ili kujiweka tayari zaidi na mabadiliko hayo. 

Alisema viwango hivi ni vya kisasa zaidi na vinaendana na maendeleo ya kiteknolojia jambo ambalolinaweza kuchangia kuimarika na kuleta usawa katika shughuli za ukaguzi wa mahesabu ya ndani, "na tunaamini viwango hivi vitachochea shughuli za ukaguzi na kuleta mafanikio zaidi ya fani nzima ya ukaguzi," alisisitiza Rais huyo wa Taasisi ya Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani nchini.

Tunajikita pia kutoa mafunzo kuelezea hasa shughuli zetu na umuhimu wake kwa jamii. "Sisi kama taasisi ya Wakaguzi wa ndani wa Tanzania tunajivunia kwamba tumefika sehemu ambapo kazi za wakaguzi wa ndani zinatambulika, japo si kwa kiwango kikubwa lakini tunaamini hatua kwa hatua tunaweza kufika mbali zaidi," alisema Dk. Njeza.

Na Elizaberth Msagula,Lindi

VIJANA waliohitmimu  mafunzo ya awali ya kijeshi ya jeshi la kujenga Taifa (JKT)  wamehimizwa uzalendo,uaminifu na uadilifu katika kusimamia na kuijenga  nchi yao.

Yamehimizwa hayo na Brigedia Jenerali Charles Peter Feluzi wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa mujibu wa sheria oparesheni ya miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Kikosi 843 Wilayani Nachingwea. 

Brigedia Jenerali Feluzi amewataka wahitimu hao kutumia mafunzo waliyoyapata katika kuijenga na kuilinda nchi  kwa kuzingatia kiapo chao huku akitaka wajiepushe na matumizi yasiyofaa katika mitandao ya kijamii na badala yake waitumie kujifunza na kwa manufaa bila kuvunja sheria na taratibu za nchi yao.

Luteni Kanali Nyagalu  Malecela ambaye ni mkuu wa kikosi cha 843 Nachingwea amesema vijana hao wakiwa kambini hapo kwa majuma 16  wameweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya awali ya kijeshi na kuwajenga vijana hao kuwa wakakamavu pamoja na wazalendo.

Awali akitoa salamu za Wilaya Katibu Tawala wa Wilaya ya Nachingwea Haji Mbaruku Balozi aliwasihi wahitimu kuendelea kujiendeleza kimasomo.

"ni kwa kupitia Elimu kijana unaweza kuwa Meneja wa Benk, Mkuu wa kikosi, Mbunge , Waziri na Hata Rais hivyo niwasihi vijana kujiendeleza kimasomo ili mfikie malengo yenu" alisema Balozi.

Nao baadhi ya wahitimu  wakaeleza umuhimu wa mafunzo hayo sambamba na kuwasihi vijana wengine kujiunga na jeshi hilo.






Peter Haule, WF, Dodoma

Serikali imesema kuwa imeunda kamati ya kukusanya na kuchambua maoni na mapendekezo ya viwango vya nyongeza ya pensheni ili kuwezesha maandalizi ya rasimu ya Waraka wa Baraza la Mawaziri kuhusu nyongeza ya pensheni kwa wastaafu wanaolipwa na Hazina.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Taska Restituta Mbogo, aliyetaka kufahamu lini Serikali itawaongezea pesheni wastaafu wanaolipwa shilingi 100,000 kwa mwezi na Hazina.

Alisema kuwa Kazi ya uchambuzi wa maoni na mapendekezo ya wadau kuhusu mapendekezo ya viwango vya nyongeza ya pensheni inatarajiwa kukamilika kabla ya tarehe 30 June 2024.

Aidha kuhusu fomula ya kikokotoo, Dkt. Nchemba alisema kuwa Kamati imeundwa na inahusisha watu mbalimbali na Wizara inayohusika na utumishi nayo inaendelea na zoezi kubwa linalohusisha masuala ya pensheni kwa ujumla wake.

Akizungumzia mafunzo kwa wastaafu wanaolipwa na Hazina kabla ya kustaafu, alisema kuwa mafunzo yanaendelea kutolewa na yataboreshwa ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma hiyo.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Taska Restituta Mbogo, aliyetaka kufahamu lini Serikali itawaongezea pesheni wastaafu wanaolipwa shilingi 100,000 kwa mwezi na Hazina.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)

Dar es Salaam, 7 Mei 2024: Programu ya CookFund inayotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Maendeleo ya mitaji (UNCDF) chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) wameandaa mdahalo wa kisera wenye kauli mbiu “Nishati safi ya kupikia na uwekezaji fedha kwenye hewa ya ukaa’ jijini Dar es Salaam.

Mjadala huu umelenga kujadili njia za kutengeneza mazingira wezeshi kwa ajili ya makampuni na mashirika ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye mnyororo wa thamani wa nishati safi ya kupikia kwenye biashara ya hewa ya ukaa. Mjadala huo ni mwanzo wa mfulululizo wa mijadala inayolenga kutatua changamoto za kisera zinazokwamisha matumizi endelevu ya nishati safi ya kupikia nchini Tanzania.

Mjadala huo ulihudhuriwa na wadau muhimu kutoka serikalini na sekta binafsi wakiwemo: Kamishna msaidizi wa nishati mbadala na umeme kutoka wizara ya nishati Mhandisi Styden Rwebangira na Seleboni Mushi, ofisa misitu kutoka wizara ya maliasili na utalii. Wachokoza mada walikuwa ni: Tajieli Urio kutoka SouthPole, Jaqueline Ngullo kutoka UpEnergy; Dr. Paul Lyimo, afisa wa uhufadhumi kutoka kituo cha kitaifa cha kuratibu biashara ya kaboni (NCMC), na Lois Kassana, mwakilishi kutoka taasisi ya sekta binafsi tanzania (TPSF).

Mhandisi Rwebangira alieleza juu ya hatua zilizochukuliwa kuendeleza biashara ya hewa ya ukaa.
“Wadau wengi hawana ujuzi wa kitaalamu wa kutosha, jambo linaloonyehsa umihimu wa kujengewa uwezo. Ninafuraha kuona ushirikiano kati ya wizara ya fedha na mradi wa CookFund kupitia UNCDF na EU katika kuratibu maeneo ya majaribio ya hewa ya ukaa kwa lengo la kutatua changamoto kupitia uidhinishwaji na uthibitishwaji.”

Kwa upande wake, Lois Kassana, mchambuzi wa sera kutoka TPSF aliainisha kuwa mipango ya biashara inatakiwa iwe na uwezo wa kukopesheka na kutoka kwa mabenki, iwe na utaalam, na uhalisi wa kibiashara unaohitajika kwa ajili ya kutengeneza fursa za masoko.

Mjadala huu ulihusisha utambuzi wa mapendekezo ya maboresha kama vile kurahisisha maombi na usajili na kuongeza ushirikiano baina ya wadau. Mkutano huo uliweka jukwaa la kubadilishana taarifa kuhusu fursa zilizopo za kuwekeza fedha kwa ajili ya sekta za umma na binafsi.

Meneja Programu na Mtaalamu mwandamizi wa Fedha kutoka UNCDF, Imanuel Muro, alisema kuwa jukwaa la maliasili ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza mjadala wa uwekezaji fedha endelevu ambao unahitajika zaidi ili kuanzisha hatua madhubuti za biashara ya hewa ya ukaa kwenye nishati safi ya kupikia nchini Tanzania.
 

Imanuel Muro, (kulia) Meneja wa mradi wa CookFund na Mtaalam Mwandamizi wa Fedha kutoka shirika la mfuko wa maendeleo ya mitaji la umoja wa mataifa (UNCDF) akizungumza wakati wa Mjadala wa kisera wa nishati safi ya kupikia na kuendeleza uwekezaji fedha kwenye hewa ya ukaa nchini Tanzania.
 

Jacqueline Ngulla (wa pili kulia), Meneja wa Operesheni kutoka UpEnergy akizungumza wakati wa mjadala wa kisera wa nishati safi ya kupikia kuendeleza uwekezaji fedha kwenye hewa ya ukaa nchini Tanzania. Kulia ni Tajiel Urioh, Mshauri mwandamizi wa sera ya hali ya hewa, fedha, na masoko ya hewa ya ukaa kutoka South Pole; Dkt Paulo Lyimo, Mtafiti na Afisa bio anuai kutoka kituo cha kitaifa cha kuratibu biashara ya kaboni (NCMC) na Lois Kassana (wa kwanza kushoto) mchambuzi wa sera kutoka Taasisi ya Sekta binafsi Tanzania (TPSF).

 

 


KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa (2024) Godfrey Mzava ,ametoa wito kwa Jeshi la Polisi Mkoani Pwani  ,kuongeza nguvu ya doria kwenye bandari bubu zilizopo kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi katika ukanda huo ili kudhibiti uingizaji na usafirishaji wa madawa ya kulevya.

Alitoa wito huo wilayani Mafia, wakati akitoa ujumbe na jumbe za Mwenge ,ambapo  Mzava amesisitiza, wale wote wanaobainika kuuza dawa za kulevya washughulikiwe ili kuokoa nguvu kazi  inayopotea.

"Ukanda wa Pwani umekuwa na changamoto kubwa ya kutumika kama lango kuu la kupenyeza dawa za kulevya ,kupitia bandari bubu zilizopo , kutokana na hilo Jeshi la Polisi muendelee kudhibiti njia zote kuu zinazotumika kupenyeza dawa hizo"

Mzava alieleza ,licha ya ukamataji wa gongo na bangi, nguvu ielekezwe kukomesha njia zote za panya zinazotumika kupenyeza dawa za kulevya ikiwemo bangi,mirungi, heroin.

Akiweka jiwe la msingi Jengo la mama na mtoto, katika Hospitali ya Wilaya ya Mafia, Mzava alisema huduma ya afya inazidi kuimarishwa wilayani Mafia baada ya Serikali kuboresha huduma za afya na kuongeza majengo mbalimbali.

Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Pwani ,Abubakar Kunenge alieleza ,mkoa unavyoendelea na mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kufanya doria na kudhibiti mianya na njia zote za panya kupitisha madawa hayo.

Alieleza ,kupitia operesheni mbalimbali kwa kipindi cha Julai 2023 hadi April 2024, mkoa umefanikiwa kukamata watuhumiwa wa dawa za kulevya 481, ambapo wameshughulikiwa kwa kuwachukulia hatua za kisheria na wengine kufikishwa mahakamani.

Kunenge alifafanua, kati ya watuhumiwa hao watuhumiwa 320 wamefikishwa mahakamani,103 kesi zao zimetolewa maamuzi, 134 taratibu za upelelezi zinaendelea bado zinakamilishwa wakati wowote watafikishwa mahakamani.

Awali Mkuu wa wilaya ya Mafia Aziza Mangosongo akipokea Mwenge wa Uhuru Mei 7,2024 katika kiwanja cha ndege Mafia alisema,  umepitia miradi 17 yenye thamani ya bilioni 2.866 ambapo miradi minne imewekwa jiwe la msingi na 13 imekaguliwa.

Kati ya miradi hiyo iliyopitiwa ni pamoja na mradi wa maji kata ya Baleni, mradi wa mazingira ( kilimo cha Mwani),mradi wa nyumba za walimu shule ya sekondari Kidawendui.

Mwenge wa Uhuru ,unamaliza mbio zake Mkoani Pwani katika wilaya ya Mafia, na Mei 8 utakabidhiwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwenge huo ,uliingia Mkoani Pwani April 29 mwaka 2024, umepitia halmashauri Tisa, wilaya Saba ,miradi 126 yenye thamani ya trilioni 8.536

 

 

 

Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita,
  Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Charles Msonde akizungumza alipokuwa akizinduwa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika mkoani Geita leo.

Kaimu Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala (wa pili kushoto) akimkabidhi mgeni rasmi na Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Charles Msonde nakala ya hotuba ya Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita.

Kaimu Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika mkoani Geita leo.

Wanafunzi wa Shule mbalimbali wakiingia kwa maandamano katika Uwanja wa CCM Kalangalala  kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika mkoani Geita.

Wanafunzi wakiwa wameshika mabango ya jumbe anuai katika Uwanja wa CCM Kalangalala kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika mkoani Geita.

Baadhi ya wanafunzi wakitumbuiza kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika mkoani Geita.

Baadhi ya wanafunzi wakitoa burudani kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika mkoani Geita.

Wanafunzi wakiwa wameshika mabango ya jumbe anuai katika Uwanja wa CCM Kalangalala kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika mkoani Geita.

Wanafunzi wakiwa wameshika mabango ya jumbe anuai katika Uwanja wa CCM Kalangalala kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika mkoani Geita.

Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita,
  Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Charles Msonde akiwa amesimama na viongozi meza kuu kuimba wimbo wa taifa kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika mkoani Geita leo.

Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita, Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Charles Msonde (kulia) akisaini kitabu cha wageni huku akipata maelezo alipotembelea Banda la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET)  kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika mkoani Geita leo.

Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita, Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Charles Msonde akipata maelezo alipotembelea Banda la Room to Read kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika mkoani Geita leo.

Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita, Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Charles Msonde, pamoja na Kaimu Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala (kulia) wakiwa kwenye Banda la CAMFED akipata maelezo alipotembelea kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa mkoani Geita leo.

Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita, Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Charles Msonde, pamoja na mwenyeji wake Kaimu Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala wakitembelea Banda la Haki Elimu wenye Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa mkoani Geita leo.

Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita, Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Charles Msonde, pamoja na mwenyeji wake Kaimu Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala wakitembelea mabanda mbalimbali ya wadau wa elimu wenye Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa mkoani Geita leo.

Msafara wa maandamano ya wanafunzi kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika mkoani Geita.

Wanafunzi wakiwa wameshika mabango ya jumbe anuai kwa maandamano kuelekea Uwanja wa CCM Kalangalala kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika mkoani Geita.

Msafara wa maandamano kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika mkoani Geita.

Wanafunzi wakiwa wameshika mabango ya jumbe anuai kwa maandamano kuelekea Uwanja wa CCM Kalangalala kwenye hafla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika mkoani Geita.


Top News