Baadhi ya watu waliookolewa katika mgodi wa Nyangarata wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wakipewa matibabu katika hospitali ya Kahama.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
WATU watano wamepatikana usiku wa kuamkia leo wakiwa hai siku 41 tangu walipofukiwa na kifusi cha mchanga katika mgodi wa wachimba wadogo wa mgodi wa Nyangarata wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa Afisa habari wa Wizara ya Nishati na Madini, Bi. Badra Masoud , watu hao waliokolewa kutoka ndani ya mgodi huo wkiwa kiasi cha mita 100 ardhini. Mmoja wao alikutwa amefariki dunia.
Kwa mujibu wa Afisa habari wa Wizara ya Nishati na Madini, Bi. Badra Masoud , watu hao waliokolewa kutoka ndani ya mgodi huo wkiwa kiasi cha mita 100 ardhini. Mmoja wao alikutwa amefariki dunia.
Bi Masoud amewataja waliookolewa katika mgodi huo kuwa ni Joseph Burule, Chacha Wambura, Msafiri Gerald, Onyiwa Aindo na Amosi Mhangwa pia limtaja aliyefariki dunia ni Mussa Supana.
Amesema kuwa watu hao wamekaa chini ya ardhi kwa siku 41, baada ya mgodi huo kudidimia kwenda chini Oktoba 5 mwaka hadi jana Novemba 15 ambapo waokoaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini walianza na kuwatoa wakiwa katika hali mbaya na kukimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Pia amesema kuwa walipokuwa chini huko wakuwa wanakula magome ya miti na kunywa maji yaliyokuwa yakitiririka na kukinga katika helmeti zao ambazo walikuwa wamezivaa walipokuwa wanaingia katika mgodi huo.
Bi. Badra alitoa wito kwa wachimbaji wadogo wa Madini kuwa wachimbe kwa kutumia vifaa vya kisasa ili kuepukana na madhara yoyote yatakayo jitokeza katika uchimbaji wa madini.
Afisa habari wa Wizara ya nishati na Madini, Bi. Badra Masoud akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO kuhusiana na watu waliopatikana wakiwa hai katika mgodi wa wachimbaji wadogo wa Nyangarata mkoanI Kahama.
Afisa habari wa Wizara ya nishati na Madini, Badra Massoud akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO Kulia ni Afisa habari wa Idara ya Habari MAELEZO, Jaiquline Mrisho.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Mungu ni mwema sana!
ReplyDeleteNashauri tulitafakari hili jambo kwa kina kidogo. Mbona imechukua muda wote huo??? Ina maana kuanzia sehemu ya kipindi cha kampeni, upigaji kura, utangazaji wa matokeo, etc. kuna watu walikuwa chini ardhini??? Ni nani walipaswa kuwaokoa, na hilo lilipaswa kufanyika ndani ya muda gani??? Katika huo mnyororo wa ukoaji kufanyike uchunguzi wa kina kwani naamini kuna watu/wadau hawakufanya kazi zao ipaswavyo.
Wanaosema wamewaokoa waache kutumia hilo neno. Huwezi kujinadi kuwa umewaokoa watu ambao wala hukuwasaidia kuishi kipindi chote hicho....na kwanza ulikuwa umeshawakatia tamaa. Aliyewaokoa, mwisho wa siku, ni Mungu peke yake!Hivyo sifa, shukrani na utukufu viende kwake tu! Alichokifanya binadamu ni kuwatoa tu kutoka huko chini, napo ni kwa msaada wa Mungu kwa huruma ya waathirika na waliozembea. Mungu ameyafanya haya kwa sababu fulani, na sio ili mradi tu. Tuyatafakari matendo yake makuu katika jambo hili.